lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu mwanajua ft dash – dizasta vina

Loading...

verse 1

alizaliwa mashariki alifahamika mahali pote
alikuwa malaika wa ndoto zetu wote
walimwita mwanajua kwa maana alijua vyote
alitamalaki nuru ilitua mahali kote

na kila mahala alipita watu walimuheshimu
hakwenda shule ila aliheshimika ka’ mwalimu
alikuwa mzuri kweli lakini shobo hana
hakuna aliyemgusa kwani alikuwa wa moto sana

urembo ulimuweka juu hakushuka anga zetu
alikuwa maarufu kushinda hata bwana yesu
hata watoto walimpenda walifanya sherehe
tuliobalehe alipopita tulimwaga mbegu

ilipofika asubuhi tulimuwaza yeye kwanza
ilikuwa ni kama desturi k*mfata
tulikuwa hatuli tukasaza
tuliwaonea wivu rafiki zake mekuli na veneranda

walikuja madogo wajanja na mapesa
wakauliza mama ukivaaje unapendeza
wakamuahidi ndizi, mawaridi na hariri
lakini jasiri rangi yake ya asili ilitesa
warembo wa dunia na vivazi vyao
waliwaza k*mfikia na ilibaki njozi kwao
wazungu walikuja na pozi kibao
walimkaribia mwisho walibabuka ngozi zao

chorus
mwanajua ..amepotea kama hakuwepo
mwanajua..ameondoka kama hakuja
mwanajua anatuk*mbusha kuwa kilichopo
kitakuwepo tu kwa muda
mwanajua…mwanajua…mwanajua…

verse 2
tulijaribu kutumia chambo
apite anase ili tuweze kutupia mambo
mitego iliwekwa aje atumbukie hapo
tuliishia k*mwona mbali na mwisho kuumia macho

haki ya nani, kuna walo’diri k*mwita mungu
walitukuza walisadiki na kuabudu
na sisi alitupa nguvu
tuweze kupambana kutafuta pesa ili tu tuweze k*mmudu

manyoka waliyavua magamba yao
wapendeze ili waje waweze kupata fao
walitanguliza vyeti na madaraka yao
waliisha kufa tukawazika na haraka zao
licha ya utofauti wake
alikuwa mkimya hakuna aliyeisikia sauti yake
wenye wivu walichoshwa na mizingu
maana alingáa sana kiasi alizificha nyota kama wingu

n*z*waza features zote complete
nilitazama sikuona diva wa ku*compete
bila ina ala make*up za kisasa
aliwaka sana.. mtoto fulani konki

chorus
mwanajua ..amepotea kama hakuwepo
mwanajua..ameondoka kama hakuja
mwanajua anatuk*mbusha kuwa kilichopo
kitakuwepo tu kwa muda
mwanajua…mwanajua…mwanajua…

verse 3
yeah!
iwapi barabara isiyo na kona?
simulizi isiyo na mwisho?
makala zimeandikwa tupo na nakala tunasoma
imeandikwa upasuka inapovuma sana ngoma

vile alikuwa amesukwa ni kwere
alipofika ilikuwa ka’ umeshushwa umeme
kwa uzuri utadhani amejiumba mwenyewe
tulihisi hatashuka milele
tulikosea kwani…zile sifa hazivai tena
imefika jioni na yeye hang’ai tena
ndege hawaimbi nyimbo, misa zimefungwa
wamwaga mbegu wote tumebaki dilemma

najiuliza, alifichwa na ndugu kwenye kaya?
au alinenepa kutoka aliona haya?
hakujua, tulishindwa kutafakari chanzo
maana alizima na hakuwa wa moto kama mwanzo

anatuk*mbushwa kuwa tayari inapofika zama
hatamu yake imefika, zamu yake imekwisha
hajaacha hata alama ya damu yake
amekufa na utamu wake yarabi nasikitika sana

namk*mbuka sababu hakudanganyika
nuru yake pahala pote ilitawanyika
toka mzizima pwani kote alipagawisha
aliondoka na mwisho alionekana ziwa tanganyika

dhahania zimeandikwa alichoka pengine
aliondoka ili w*ng’ae nyota wengine
itakufa damu, itakufa nyama
nenda mwanajua nenda tutak*mbuka sana

chorus
mwanajua ..amepotea kama hakuwepo
mwanajua..ameondoka kama hakuja
mwanajua anatuk*mbusha kuwa kilichopo
kitakuwepo tu kwa muda
mwanajua…mwanajua…mwanajua…

lirik lagu lainnya :

YANG LAGI NGE-TRENDS...

Loading...