lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu mikasi – mangwea

Loading...

ni asubuhi ninaamka ninapiga mswaki
kisha naenda kubath kuweka mwili safi
narudi ghetto nafungua kabati

nachukua pamba bling bling kwa chati
na t-shirt ya black na jeans ya khaki
na chini nina simple white tisha za nike
kisha mzee najipulizia marashi
nanukia safi
niko na machizi wa chambers squad na darky
tunawapigia simu rich coast wako wapi
tunakutana mitaa ya chaga bite
asubuhi tunapata zetu supu kwa chapati
na mitungi ya kupotezea wakati
ukitaka fegi mezani kuna pakti
iwe sport au sm au emb-ssy
hapa utakula raha mpaka mwenyewe utasema basi
tunakamua mpaka ile mida ya lanchi
tunaagiza ugali mkubwa na samaki
makamuzi yanaendelea mpaka nighty
watu wanaingia graveyard kwanza kupata nyasi
tunarudi kila mmoja anajisachi
ni kiasi gani mf-koni kilichobaki
kujicheki mi nina kama laki
nikawaambia machizi kinachofuata mikasi

mitungi, blanti, mikasi
kama ukitaka kuvinjari nasi
basi mf-koni mwako nawe uwe safi

mitungi, blanti, mikasi
kama ukitaka kuvinjari nasi
basi mf-koni mwako nawe uwe safi

kulewa tushalewa kilichobaki mikasi
washikaji milupo tutapata wapi?
milupo labda mitaa ya kati
so tunaenda vipi kwa miguu au kwa basi?
usiku huu bora tuchukue taxi
poa basi tusipoteze wakati
ks ks naita taxi
njoo utupeleke mitaa ya kati
tukacheki midudu ya kupiga mikasi
tuelewane kabisa itatucost shilingi ngapi?
(buku nne tuu) aah wapi!
kwani hapa na pale ni umbali wa hatua ngapi?
(si mnacheki wenyewe mko w-ngapi?)
usimind sana babake tuko safi
tuchangeni tusipoteze wakati
ludi eh kwani we una shilingi ngapi?
(buku tano) venture? (bati)
sasa wewe una bati usiku huu unaenda wapi
wakati hiyo bati hata soda tuu hupati
bora uweke kesho unywee chai na chapati
asiye na kitu mi naona bora akabaki
tusije mbele tukashikana mashati
suka eh! tuanzie masaki
mchizi kapiga simu yani kuna bonge la party

mitungi, blanti, mikasi
kama ukitaka kuvinjari nasi
basi mf-koni mwako nawe uwe safi

mitungi, blanti, mikasi
kama ukitaka kuvinjari nasi
basi mf-koni mwako nawe uwe safi

dereva funga brake tushafika kwenye party
eeeh bwana eh k-mbe bonge la party
cheki mademu kibao utadhani kitchen party
duh! cheki lile anti lililovaa skintight
ee bwana eh! liko safi
sio mchezo babake unaweza ukahonga laki
aah wapi! mtu kama mi hanipati
usawa wenyewe huu wa kulenga kwa manati
haya basi tujichanganye katikati
tukacheki mitungi na mademu wa mikasi

oh yeah, braza mwenye black unaitwa na yule anti
‘yuko wapi?’ yule aliyevaa suti ya kaki
aunty vipi?
aah safi. samahani kwa kukupotezea wakati
nilikuwa naomba tuwe wote kwenye party
au unasemaje? (mi naona safi)

samahani wewe anti ambaye umevaa shati
hivi unaitwa nani eh? naitwa bahati
hivi aunty nishawahi kukuona wapi?
acha longolongo we sema una shilingi ngapi

oyaa we’e vipi? mpango wako vipi?
mbona mi mazee mpango w-ngu safi
ishakuwa usiku twenzetu tukachukue taxi
(aha) twenzetu tukapige mikasi

mitungi, blanti, mikasi
kama ukitaka kuvinjari nasi
basi mf-koni mwako nawe uwe safi

mitungi, blanti, mikasi
kama ukitaka kuvinjari nasi
basi mf-koni mwako nawe uwe safi

yeah, yeah, yeah, yeah east zu yo! holler
bongo records
ngwair
ee bwana eh
niko around mazee

lirik lagu lainnya :

YANG LAGI NGE-TRENDS...

Loading...