lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

a confession of a mad father - dizasta vina lyrics

Loading...

nilimwambia hakuna kitu ataniambia
nikifa hakuna kitu nitamwachia
nilimwambia anaitia aibu familia
nilipenda mtoto ila tangu nimzae nilijutia

nilimwambia anastahili fimbo
anastahili msiba mbaya usio na maziko
asikae mezani asishike sahani au kijiko
asitumie jina langu la mwisho
nilimchukia sana

nilimwambia asiniite baba
aliponiita hata bahati mbaya nilimchapa
sik*mpa mahitaji, hamu ya mtoto iliniisha ghafla
alianza shule sikulipa ada

waliponiuliza nilimkana hadharani
nikasema hata kufanana hatufanani
nilimwambia simpendi ni bora ningezaa hata nyani
nilitamani nimgawe kwa jirani

nilimpeleka kwenye misa za kilokole
nilimchapa viboko vya kutisha kwa mkole
habari zake zilitambaa nilipewa pole
nilihama mitaa kuepusha watu kuninyooshea vidole
nilimuwekea mifano kadhaa ya kubuni
kwamba kuliko yeye bora ningezaa hata mhuni
nilimwambia namwona kama chawa au kunguni
aliniponigusa bahati mbaya nilinawa kwa sabuni

sik*mpenda nilihamishia chuki kwa mama yake
niliona laana kuleta mtoto wa aina yake
sikutaka k*mwona wala k*mjua katu
na nakiri nilishajaribu k*muua mara tatu

hakuwa na marafiki tulimtenga ndugu
tuliamini ilikuwa ni laana toka kwa mungu
alinikimbia sikutaka kusikia sauti yake
sikuwa tayari kuuafiki utofauti wake

tulimweka kwenye taasisi bila idhini
alelewe akifanyiwa uhakiki wa kidini
kilichofanya nimwone ni mzigo mara mbili
ni pale taasisi zilipomshindwa k*mbadili

tofauti ya haiba na hisia
sikuwa tayari kamwe kuukubali uhalisia
achana na vipigo vikali k*mnyima chai
ilibakia kidogo nimzike akiwa hai

nilikomaza chuki kwa kutumia jadi na dini yangu
au itikadi ya jamii yangu
nilifurahi kuona hana mahala pa kwenda
maana sio marafiki hata ukoo ulimtenga
hawakutaka wakae naye
vitabu vya mungu vilishauri auwawe
nilikesha kuomba mungu aibadili tabia yake
alipopita karibu nilimtemea mate

nilimwita majina ya kutosha ya kishezi
mara boga mara mboga mara shoga mara ndezi
mara mzoga, nyoka asiye nyooka kwa malezi
nilitamani hata nafsi ingemtoka niimbe tenzi

niliamua kufanya maamuzi magumu
nikamfunge porini kisha nimnyweshe sumu
nikaandaa nyezo nikanunua na kamba
nikaenda chumbani nikakuta barua kwenye kitanda

inasema
mi ni mtumwa wa maumbile kiasili
iliyonizidi nguvu kihisia kiakili
natamani ingekuwa rahisi kubadili
na kwa bahati mbaya baba hukuwa tayari kujadili

nisamehe sana baba
muda hautoshi kukuomba msamaha mara saba
kwakuwa nimeshindwa kuwa jinsi we unataka
najitoa uhai ili nikuondolee dhihaka

Random Song Lyrics :

Popular

Loading...