
kesho - dizasta vina lyrics
verse 1
kesho nafasi ya kuanza upya
k*maliza kuishi nafasi ya kuanza kufa
kuivunja sheria nafasi ya kufuata ruksa
kuik*mbuka jana au kuanza kuifuata future
future ni leo siku ambayo miti hukimbia
jua hushuka upendo, marafiki hufifia, (hufifia)
wimbi la wanafiki huingia
kesho ya tumaini hubakia
tumaini, shika walau shika walau
na ujifunze kuziba kombe pindi anapopita nyang’au
akishapita tenda wema halafu kisha sahau
na uchunge unaponena watakuzika wadau
wadau, walikua uchi ukawavika mavazi
nyumba yako ikavunjika wakakunyima hifadhi
je, utasamehe utasahau kulipa kisasi
au kesho itakukuta umeshika risasi
risasi inawaza wapi itakukutia kesho
utatoroka kambi ama utavungia ghetto
tusipofikia lengo, utahama ukoo kwa kitu kidogo au utaitumikia nembo
nembo ya mjeshi ninayekaza mwendo kishujaa
kama unavyokaza nyonga kwenye tendo la zinaa
napiga goti nashukuru uwepo wa sanaa
kihisia nawapeleka kesho majamaa
majamaa walikua wavivu hawakukazana
waliishia kuamini kuwa kuna wingu la laana
waliseti mipango ila siku hazikufanana
huwezi kuikabili kesho kwa mbinu za jana
Random Song Lyrics :
- freak side - bei maejor lyrics
- vita nomade - diaframma lyrics
- sua mãe - fbc & iza sabino lyrics
- the truth - the jets (group) lyrics
- taught to lie - samantha crain lyrics
- puls des lebens (syrian mix) - endanger lyrics
- a satisfied mind - mahalia jackson lyrics
- blutgeld (part i) - cyborg attack lyrics
- on a high (jamie myerson club mix) - duncan sheik lyrics
- mystery train - litfiba lyrics