
dunia ina mambo - eric wainaina lyrics
shetani akamwuliza mtakatifu petero
umewahi kuangalia huko chini (aye aye)
mtu maskini akiiba mkate
atavalishwa pingu miaka minne (aye aye)
lakini tajiri anayezorotesha
umaskini wa nchi nzima (mwajijua)
anachekacheka na hakimu
baadaye wapo wote pamoja mikahawani
dunia ina mambo
kweli ina mambo
dunia ina mambo
dunia ina mambo
nyuma ya kila mlango
dunia ina mambo
shetani akamwuliza mtakatifu petero
ni dini gani inayoendeleza chuki (mambo bado)
kwa ajili ya bidii ya bin adam
mimi sina kazi (mambo bado)
warumi wachukia wakristo wengine
wengine wachukia waislamu (bure bilash)
waislamu wachukia wayahudi
na nguvu zangu zote singeweza hayo yote
dunia ina mambo
kweli ina mambo
dunia ina mambo
dunia ina mambo
vituko na vichekesho
dunia ina mambo
shetani akamwuliza mtakatifu petero
ni kulala mnalala au vipi (hallo hallo)
mnaruhusu viongozi wa nchi tajiri
k*miliki nchi masikini (hallo hallo)
kwa mfano wananchi wa nchi zilizokuwa chini ya ukoloni
waliporwa mali zao au siyo (au siyo)
basi mbona walionyanyaswa wasipande ndege
na kwenda ng′ambo ili kurudisha haki zao
dunia ina mambo
kweli ina mambo
dunia ina mambo
dunia ina mambo
mbele ya kila wazo
dunia ina mambo
dunia ina mambo
kweli ina mambo
dunia ina mambo
dunia ina mambo
mbele ya kila wazo
dunia ina mambo
dunia ina mambo
kweli ina mambo
dunia ina mambo
dunia ina mambo
vituko na vichekesho
dunia ina mambo
Random Song Lyrics :
- yes i have eaten so many lemons yes i am so bitte - bar italia lyrics
- greatest love - anna luther lyrics
- the fascinating world of speed cubes 3x3 - martin lyrics
- but... - syarahhhhhhh lyrics
- вчерашнее завтра (yesterday's tomorrow) - blago white lyrics
- zombie - atzbr lyrics
- tələbə - elmira rəhimova lyrics
- balaclava babies - sik-k & haon lyrics
- north country ride - the milk carton kids lyrics
- no justice - pepto b lyrics