
dunia - harmonize lyrics
nikifikiria dunia huwaga sipati jibu
nawaza mpaka nadata
nikikuuliza nini dunia huwezi kunipa jibu
hapo ndo napata utata
mmmh muda mwingine unaweza dhani ni utani
mbona vitu vizuri vyote viwe ni vya shetani
eti mziki shetani, pesa nazo shetani
mpira na pombe shetani
mademu na mihadarati, shetani
naamini mungu yupo najua
ndo ananifanya ninapumua
akitaka hata sasa ananichukua
ila mi nataka kujua
ni nini dunia
dunia dunia
hivi ni nini dunia
dunia eeh
mmmh wanaoishi kwa imani
misikitini makanisani
uwepo wao hauonekani
hali zao zipo taabani
hivi ulikuaga wapi before
hujaja duniani
na kwanini kunakifo
unapokwenda hapajulikani
sawa safari ni yetu sote
na hakuna aliyekwenda na akarudi
j*po kutusimulia
kama pazuri ama pabaya
uwe tajiri ama masikini
kwa mchanga utarudi
minatoa wosia
tusiishi kwa ubaya
kunakidude kinaitwa mapenzi
hakijawahi kueleweka
wakati wewe unalia
mwenzako yeye anacheka
hivi ni nini dunia
dunia dunia
ni nini dunia
dunia eeh
eeh pedezye k*mbuka
msalimia mwijaku
tuombeane mwisho mwema (eeh eeh yeah)
tuombеane mwisho mwema (maana hakuna anaejua kеsho)
tuombeane mwisho mwema (kama wewe muislamu)
tuombeane mwisho mwema (omba kwa dini yako)
tuombeane mwisho mwema (kama wewe ni mkristo)
tuombeane mwisho mwema (nisiri nisiri)
tuombeane mwisho mwema (tuombeane nisiri)
ni nini dunia
dunia dunia
hivi ni nini dunia
Random Song Lyrics :
- jimbo (acoustic) - fredo disco lyrics
- unborn - binary code lyrics
- canção ao violão - fredi bessa lyrics
- кишка кишке (kishka kishke) - мистер малой (mister maloy) lyrics
- блезир (for the species) - mirs lyrics
- my dream girl is my ex now - sam setton lyrics
- keep a tec - smokepurpp lyrics
- virgem - mc henny lyrics
- give - nils lofgren lyrics
- hamatzav hakashe - המצב קשה - shalom hanoch - שלום חנוך lyrics