rebekah - maralee dawn lyrics
wakati mwingine nikiketi kukuimbia mie
huwa nalemewa kupata maneno yanayoshimiri
ni kama mtoto mchanga anapojaribu kueleza ukubwa wa sayari
ni kama kidege kinapojaribu kueleza upana wa mbingu
ni kama changarawe kujaribu kueleza ukubwa wa bahari
ukweli ni kwamba maneno yangu hayatoshi, hayawezi kueleza
hivyo daima na milele siku zote za maisha yangu
nitatafuta kukuimbia maneno yanayokufaa
wakati mwingine nikiketi kukuimbia mie
huwa nalemewa kupata maneno yanayoshimiri
ni kama tone la maji kujaribu kueleza mfuriko wa mvua
ni kama wapendanao kujaribu kueleza fumbo la penzi
ni kama mshumaa kujaribu kueleza kung’aa kwa jua
ukweli ni kwamba maneno yangu hayatoshi, hayawezi kueleza
hivyo daima na milele siku zote za maisha yangu
nitatafuta kukuimbia
maneno yanayokufaa
ni kama jiwe linapojaribu kueleza urefu wa mlima
ni kama sheha shupavu kujaribu kueleza hadithi zote za jadi
ni kama mwenye dhambi kujaribu kueleza neema ya msamaha
ukweli ni kwamba maneno yangu hayatoshi, hayawezi kueleza
hivyo daima na milele siku zote za maisha yangu
nitatafuta kukuimbia, nitatafuta kukuimbia
maneno yanaykuofaa
Random Song Lyrics :
- espero que seas feliz - nemesis 666 lyrics
- ready - july 7 lyrics
- après la pluie - jaures lyrics
- dil - sadphly lyrics
- ready - t'antum lyrics
- befreit durch deine gnade - feiert jesus! & katrin lauer lyrics
- funny - alex stanilla lyrics
- second hand - m.anifest lyrics
- elite - loner nba lyrics
- eden - helldvck & percøgvng lyrics