lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu rastaman – daz baba

Loading...

[intro]
oh rastaman
iré rastaman

[verse 1]
watu wengi wajiuliza nini maana ya rastaman
elewa haya ni maisha ya mtu mwenye imani
iwe ya msikitini au ni kanisani
au umwabudu jah au mola kutoka moyoni
nami nawashangaa hawa tunawaita viongozi wa dini
mbona kila siku ndio wana kesi za ugoni
halafu pekee yao wanajifanya waumini
kama ni waumini basi dini alileta nani?
nnavyojuwa mwalimu dini alileta mkoloni
kipindi kile babu zetu wakiwa utumwani
ndipo tulipo fundishwa dini na white man
ila kabla ya hapo dini yetu ilikuwa imani
tulisali, tukaabudu (?) maporini
na mvua zikanyesha huko mashambani
tukapata mahitaji tukakidhi kinywani
iweje dini ya watu wote useme huja iman

[chorus]
iré jah
iré jah
iré rastaman
hizi ni salamu zetu kutoka zamani
tuungane masela w*ngu na ma*rastaman
tuungane na watu wote sasa’ wenye iman
iré jah
iré jah
iré rastaman
hizi ni salamu zetu kutoka zamani
tuungane masela w*ngu na ma*rastaman
tuungane na watu wote sasa’ wenye iman
[verse 2]
nitazidi itetea ngozi ya mweusi jamani
sababu ndio asili ya watu hapa duniani
kama unabisha’ kaa tazama olduvai gorge ndani
ndipo lilipo onekana fuvu la kale hapo zamani
pia tulikuwa na vitu vingi vya thamani
kachukua mzungu raw material kwake viwandani
tukabakia afrika ‘sisi masikini
bara letu wakaliita tena ni la gizani
waliwauza babu zetu kama nyanya sokoni
wakawachapa mijeledi uchi hadharani
kitu kulipa kisasi hadi leo mi sidhani
ndio maana mimi mwenzenu ninaishi kwa imani

[chorus]
iré jah
iré jah
iré rastaman
hizi ni salamu zetu kutoka zamani
tuungane masela w*ngu na ma*rastaman
tuungane na watu wote sasa’ wenye iman
iré jah
iré jah
iré rastaman
hizi ni salamu zetu kutoka zamani
tuungane masela w*ngu na ma*rastaman
tuungane na watu wote sasa’ wenye iman
[verse 3]
dini nyingi za sasa’ sadaka kwanza mkononi
nitatoa nini rastaman’ mimi masikini
kama dini inauzwa niambie ni bei gani
ili nichange, change nisije fika motoni
vipi asingiziwe huyu kwa kesi ndogo jamani
mbona sisi hatusemi hata waabudu uchi vyumbani
hata kama ni dini basi na hizo dini gani?
mimi nnavyojuwa wanamtukuza babylon
nimeshachoka k*mtumikia kafir’ shetani
ndio maana mambo haya nayaweka hadharani
kama nime wakosea waumini samahani
ila ningependa watu wote dini iwe moja iman

[chorus]
iré jah
iré jah
iré rastaman
hizi ni salamu zetu kutoka zamani
tuungane masela w*ngu na ma*rastaman
tuungane na watu wote sasa’ wenye iman
iré jah
iré jah
iré rastaman
hizi ni salamu zetu kutoka zamani
tuungane masela w*ngu na ma*rastaman
tuungane na watu wote sasa’ wenye iman
[hook]
iman
iman
rastaman
dini iwe imani
iman
iman
rastaman
dini iwe imani

[chorus]
iré jah
iré jah
iré rastaman
hizi ni salamu zetu kutoka zamani
tuungane masela w*ngu na ma*rastaman
tuungane na watu wote sasa’ wenye iman
iré jah
iré jah
iré rastaman
hizi ni salamu zetu kutoka zamani
tuungane masela w*ngu na ma*rastaman
tuungane na watu wote sasa’ wenye iman

[outro]
scout jentaz
p*funk
bongo records, daz nundaz
yeah, yeah
rastaman
i and i

lirik lagu lainnya :

YANG LAGI NGE-TRENDS...

Loading...