lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu siri ya mchezo ( the game’s secret ) – fid q

Loading...

nilipotoka mbali na ninaheshimu nilipo/sikuwa na umuhimu kihivyo… stimu zikanipa elimu ya biko/ kimaandiko… kimistari.. hadi fans wanascream nikirap../ sikuamini kama nina zali mpaka nilipoidream hiphop/
wanapagawa…. na baadhi ya mambo nayoyajua.. pia nina uwezo wa kufanya mpaka madawa yanaugua/
wanapagawa na nyimbo ngumu hawa #teammabiiitoz /
achana na power window.. sijui rimz za dimpoz/
haileti bingo, mshiko? star ishi simple/ sanaa iko hivyo sometimes.. hukataa kukaaa ulipo/
wanaodharau.. hujiletea matatizo..hawajui kama wadau… hupendelea kukuona hivyo?/ bonge la staa.. donge la njaa.. hauna kitu/
jikombe ugongwe…mtaaa ukuone hauna ishu/
ukishindwa kujiandaa… jiandae kushindwa/mjinga utaachwa unashangaa k-muona martin kadinda/ usmati anaotinga, majumba mandinga ya bwana almasi.. je hizi track za harakati ni ujinga?/
hapana…. nguvu ya mamba ni maji/ na umaarufu au kutamba.. kushika namba ni bahati..sio kipaji kama kubanda eti unachana kigumu/ kisa track ikivuma sana kwenye chati haidumu /
amani kwa chachage na makuwadi wa soko huria../ baba asante kwa utafiti na zawadi ya almasi ya bandia/nyumbani… nasikiliza dunia ya sasa ya marijani../ najiuliza tutarithi nini ikiwa imani ishakwisha tangu zamani?/ labda kubisha na wakinitisha najihami../ inasikitisha unapoibiwa na aliyekupigisha ni jirani/
‘’ pole maprosoo’’ ( uhujumu –uchumi ) umefanya umetubu.. / wazee ni wahuni hadi soo waay back before sugu/
taifa la kondoo.. huendeshwa na serikali ya dubu/ na mbwa mwitu wenye siri.. ili bepari umuabudu/ kimahakama, kiserikali, kidini umsujudu../ huo ni utumwa pia/unafanya vijana wanaumia../ tunaishia kufia mabatani kama nzi ndani ya gl-ss ya bia..

chorus: ( juma nature )
siri ya mtungi aijuaye kata../ komaa… kaza.. kisha utapata/ x 2
siri ya mchezo naijua mimi.. tu.. na hakuna mwingine x 2

verse 2:
tofauti ya biashara na siasa ikila hasara inaweza buma/ wakati siasa kila mara ukiwa unang’ara ujue kuna.. kinara/ anayeunda msafara wa wanaojituma na kuchuma kwa kukufanya uwe imara hapo hasara hakuna/ kidumu chama cha masela… ukoloni mambo leo umetupa uhuru wa bendera,/
tuone kufuru za wenye hela/
tanzania ni ‘ demu wa mtungo ‘ wanamuiita cha woote/’’ hangover .. ‘’anaikimbia kwa kupiga ‘ “ mtungi “ saa zote /mkubwa anazuga atasolve… matatizo ya nchi yake/ ‘’na gari bovu..’’ halisuk-mwi kwa kukaa ndani yake/ maendeleo ni ile ndoto..mwezekaji ashaipuuza../ je kukaa karibu na moto ni kuuota au kujiunguza? / hakuna uhuru wa kweli (africa) msidanganywe na illusion/ na daily tunafeli sababu ya political inst-tutions/
civilization imeadvance sasa wanatuua economically../ hakuna utumwa mbaya kama ule wa kujiona uko free/ kuusaka ukweli ni sawa na k-menya kitunguu/ kila ganda litakutoa machozi na utabaki macho juu/ukishafika kwenye kiini niambie nini utagundua..? zaidi ya mafaili yaliyounganika utaghairi kuyafunua?
wamejivisha u-noah.. safina zao zikatoboka/
wakajivisha u-mussa.. fimbo zao hazikugeuka nyoka/
sasa wanaujaribu u-mungu mtu kuamua nani leo atatoka….!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!???????????????????

lirik lagu lainnya :

YANG LAGI NGE-TRENDS...

Loading...