lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu mama – nay wa mitego

Loading...

niko fresh niko poa
asante mungu kwa pumzi nayopumua
nakuombea mama umenileta kwenye dunia
leo utafurahi kidogo mi nawe tukiongea
kwanza pole kwa msiba baba ametangulia
najua una kazi nzito ya kuongoza familia
kabla baba kufariki kuna mambo yalitokea
wapo waliopenda wengine walichukia
mama huenda baba anajua ni ukoo moja
ila mama we na baba najua si kitu kimoja

umejaliwa hekima busara na upendo
inshallah tutafika mbali usipo badili mwenendo
kuna baba wadogo hawa kuwa nao makini
bado hawaamini kama ndo umeshika mpini
waongo wanafiki wamejawa ufitini
wanaongoja uteleze ili wakupige chini

hey mama we love you mama
hey mama tunakupenda sana
hey mama we love you mama
hey mama tunakupenda sana

tukificha maradhi kifo kitatuumbua
mama tusipoziba ufa hakika tutajenga ukuta
kuna mambo ya msingi ni lazima kuyaongea
mama sio kwa ubaya ni kujenga familia
baba alikuwa mkali mama mwеnyewe unajua
yaani tuliishi kwa taabu j*po kuwa ni wa kishua
sio sisi tu mpaka wageni walikimbia
kuhusu kaka yangu ibra natumai ulisikia

nayе alikimbia ameacha mke na watoto pia
wengine walipotea tu hatujua wako wapi?
sema neno kuhusu hili mama ututoe wasiwasi
mama njaa ikiuma tunaruhusiwa kusema
ukikosea tunaruhusiwa kuongea
au ndio kama baba mtu mzima hakosei?
nina zawadi yako siku yako ya birthday

hey mama we love you mama
hey mama tunakupenda sana
hey mama we love you mama
hey mama tunakupenda sana

mama hili la mwisho
najua unajua kwamba, ukishatengea na familia yako
huruhusiwi na unapoteza sifa za kushiriki kwenye vikao
vya maendeleo ya ukoo

lakini shangazi halima na wenzake
mbona bado nawaona kwenye vikao vya ukoo?
na walishatengwa na familia yao?
sema kitu kuhusu hili mama
all the best mama
wajukuu zako nyumbani wanasubiri
nirudi na chochote kitu
acha nikatafute

hey mama we love you mama
hey mama tunakupenda sana
hey mama we love you mama
hey mama tunakupenda sana

lirik lagu lainnya :

YANG LAGI NGE-TRENDS...

Loading...