lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu amen – rapcha

Loading...

[verse i: rapcha]

uh hebu tazameni
matendo ya mungu yanavyotisha
amefanya mengi makubwa ya kustaajabisha
marafiki leo wana upendo kesho umekwisha
ila upendo wa mungu hauwezi kwisha

naamini neno lako linaishi forever
utendawazi hauwezi kubadili
dhambi ikawa haki, never!
umenifikisha sehemu ambazo
wala sikuwahi kuzifikiria
sifa zako nitazihadithia

unaniepusha na maadui
unanilinda na mabaya
ambayo hata siyatambui
mungu uliye hai
hata mimba zilizotokea
kwenye mazingira ya dhambi
watoto umewapa uhai

na kama pumzi unanipa bure
sasa kivipi tamaa ya pesa initenge na wewe
nashukuru kwa kunileta hii sayari
milele nitakuamini mungu wa kweli amina
[chorus: lady jay dee]

amen baba, amen
upendo wako, huruma yako amen
wema wako utukufu wako, amen
amen baba, amen

[bridge: lady jay dee]

umenipa maarifa, umenipa uhai, umenipa mali
hata nacho kipaji siwezi sema sijaridhika
umenipa kile ulichonipa, hukunitupa
nami sitakijuta baba, nasema amen

[verse ii: rapcha]

glory to god, utajiri mkubwa ni furaha
mungu anaweza kubariki mpaka ukashangaa
niwapo kwenye njaa nik*mbushe kwamba
ndege hawalimi, hawavuni ila hawakosi chochote

nilipotoka usiache nik*mbusha
nipe hekima nisitamani magari
nisiyoweza kuyaendesha
niishi kwenye ukweli nidumu
maana uwongo hauishi milele
na unaua faster kuliko sumu
pia asante kwa kunipa bidii
napokuomba haujibu haraka
unajibu wakati sahihi
una hekima inayoshangaza dunia
watu hata tungombane vipi
tunashare mvua na jua

nilijalie nisilewe sifa
nik*mbuke siku za uhai w*ngu zinahesabika
hivyo nikuabudu nikiwa kijana
nawe utaniweka juu kwa baraka leo zaidi ya jana

[chorus: lady jay dee]

amen baba, amen
upendo wako, huruma yako amen
wema wako utukufu wako, amen
amen baba, amen

copyrights: bongo records tanzania

lirik lagu lainnya :

YANG LAGI NGE-TRENDS...

Loading...