
amen remix - rapcha lyrics
Loading...
verse 1: {rapcha}
nilipohisi upweke kwenye moyo na mawazo kunichakaza
wanadamu nikawaomba msaada wakanitangaza
nikainua macho kwako, ukaniambia mwanangu nikabidhi shida
ukanifuta chozi nikanyamaza
sina cha kulaumu
neno lako ladumu
nikikuamini una rahisisha nnayoyaona magumu
umenipa muda mrefu wa kujaribu kujirekebisha na kutubu dhambi kabla haujanihuk*mu
kazi za dunia zinafanya nikusahau
na ninasahau kuwa we ndo unae nipa nguvu ya kuzifanya
lakini bado unanipenda sana
ungehesabu makosa yetu hakuna ambaye angebahatika kukuona
kukuamini inabidi
uliruhusu nif*kuzwe kazi ili unipe nzuri zaidi
unajua hamu niliyonayo ya kuiona pepo
nijalie nife kwenye imani ntapofika mwisho
amen
Random Song Lyrics :
- umloufbahn - patent ochsner lyrics
- what's yesterday - dean martin lyrics
- más allá - abram lyrics
- rostra - cicero the roman republic lyrics
- firing line - moon martin lyrics
- drugs (version iv) - kool keith lyrics
- jealousy - 3 cards marley lyrics
- shoppin' for clothes - the coasters lyrics
- gusto - drk gry lyrics
- tame a wild one - jj grey & mofro lyrics