lirikcinta.com
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu hujambo mwanangu – rostam (tz)

Loading...

it’s rostam baby
maa…(tongwe records bby)
bin laden

nakusalimia kwa jina la jamhuri ya tanzania
siku nyingi hatujaongea na sisi ni familia
na mbona hukuja k*mzika baba, kwa nini?
ukipata muda kasome luka 9 mstari wa 60
we nae umezidi utukutu ndio maana baba alikuchukia
wengi tulioko huku mioyo yetu iliumia
kuona baba akiwakemea waliotuonea aliwasifia
mwenzangu ulipendwa sana, nyimbo zako alifurahia

ulideka ulipewa zawadi ya t*shirt na kofia
kaka marehemu hasemwi njoo tujenge familia
acha niondoke nina damu ya kunguni nisije nikajifia
tunaimba wote nafungiwa mimi? umesahau ya kibamia?

ila sasa unaweza ukarudi (mmh)
mbona mambo yako shwari (no)
hata kaka aliyekuwa hakupendi
mambo yake yako mshazali (wacha)
aliuza nyumba ya kino bila hela ya udalali
akapata ya kigamboni kasombwa na upepo wa bahari

hii ni hatari kuna watu baba aliwapa kiburi
tulionekana wajeuri kila tulipo mshauri
eh eh kaka eeh basi rudi uf*kue kaburi
no na wasiwasi na walio baki mama awaangalie vizuri
kama? kaka yetu aliye hai na yuko happy? yule chenga
polepole haya mambo sasa ni msiba
njoo chemba (narudi januari na nitafika kwa kaka bumbuli)
hata kwa mamdogo yule mwalimu wa tanga utaishi vizuri
mama tuna kutazama we
mama tufute machozi
mama mama mama
rudisha tabasamu

kila mtu anasema lake hivi kipi kime muua baba?
achana na maneno ya watu na tena badirisha mada
ni maradhi ya moyo usisikilize hizo kelele
muache baba apumzike kwenye nyumba ya milele
okay, na mama anaendeleaje yuko dar au yupo mkoa?
tafadhali msisitize asiache kuvaa barakoa
mama yako yupo majuk*mu ndio yamembana
na juzi kwenye kikoba wamempa uwenyekiti wa chama
na nimewapenda sana wale wasaidizi alio wachagua
waliopita ni wezi wa vikoba yani afadhali amewatimua
na kikoba cha vijana bado anakiongoza kaka
mmh yule sidhani kama mama atamuacha nina mashaka

hivi vipi huko umeshaonana na dada?
maana hata yeye ilikuwa haziivi na baba
dada amechoka wanafamilia wana mw*ngusha
ila nitaonana nae sisi ni ndugu siwezi k*msusa
shauri zenu bwana tukipewa urithi msishangae
nyie si mmegoma kurudi tusilaumiane baadae
emhee yani toka nikujue leo mdio umeongea cha maana
nina mengi ya kukuuliza smije mkamdhulumu mama
vipi swimming pool ya babu ile ya rufiji?
sasa hivi iko chini ya nani na inamnufaisha bibi?
baba alisimamia katuachia sisi wanae
na k*mewekwa mataa yanayo imulika kisarawe
na ile biashara ya bagamoyo baba alioisitisha?
juzi mjomba alisema iendelee inasikitisha
kwa hiyo kamsaliti baba eh? ah ah sijamaanisha
mama amuw*ngalie kaka yake kwa makini atamfelisha

mama tuna kutazama we
mama tufute machozi
mama mama mama
rudisha tabasamu

baba alifanya mema mengi muacheni alale
oya saa ngapi huko? unasikiliza ngoma za kale?
natamani kuisikiliza ya kwelina kwenye daraja la mfugale
huku saa 8 nina mawazo hivi njiwa bado wapo wale?
njiwa wametutia hasara sijui aliwaza nini baba?
kivipi? wakati naondoka mi niliwaacha wako saba
(mama akaongeza watatu) njiwa mkubwa hatagi kwa nini?
lile banda kule kijijini sa baba alilijengea nini?
ila nitunzie sana mamangu bado ulinzi anauhitaji na kingine
(mwe makini na yule baba mdogo mchungaji)

mama yupo sehemu salama usijali punguza uwoga
na ushauri pia anapewa na baba mkubwa wa msoga
halafu baba na yule uncle wa singida hawakupatana
kwa nini wasikae wamalize tu tofauti zao na mama
ndio uongee nae sasa harudi si unajua kuwa alihama
yeye na rafiki zake wapate usalama
na wale nashangazi wawili bado wana hasira na baba
w*ngesamehe na kusahau w*ngempa mama msaada
na umwambie mama aendelee kushirikiana na majirani
familia ina amani waliokwazwa warudi nyumbani
naona kikao cha familia kina ndugu wa upande mmoja
uncle anawajibu ndugu wa nje na kuacha kujadili hoja
ebu kwanza ngoja mama anaingia tutaongea baadaye
nitakucheki ngoja nimpe simu uongee nae

“halloo hujambo mwanangu….”

lirik lagu lainnya :

YANG LAGI NGE-TRENDS...

Loading...